May 2, 2017
Timu ya Liverpool inazidi kujitengenezea mazingira ya kuingia kwenye nne bora ya msimamo wa England baada ya kuichapa Watford bao 1-0.
Bao la Emre Can aliyefunga katika dakika ya 45 limeifanya Liverpool kusonga mbele kwa pointi 69 na kuwabwaga Man city, Man utd na Arsenal.
Liverpool inatakiwa kushinda michezo mitatu iliyobaki dhidi ya Southampton, West Ham na Middlesbrough ilo kujihakikishia nafasi ya kuingia kwenye nne bora.

Comments
Post a Comment