Manula awaondoa wasiwasi mashabiki wa Azam.


Golikipa namba wa timu Azam amekanusha madai ya kujiunga na timu ya Simba kama zilivyokuwa zimeenea baadhi ya taarifa kuhusiana na kipa huyo kusaini Simba.

Manula kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwatoa hofu mashabiki wa Azam kuwa kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kusaini dili jipya.

Manula ambaye ambaye ni kipa bora wa VPL 2016/17 alipigiwa simu nyingi baada ya kuenea kwa taarifa za kujiunga na wekundu wa Msimbazi.

Comments