May 19, 2017
Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Salum Mayanga ameandaa kikosi tayari kwa ajili kupiga kambi mei 23, mwaka huu.
Hatua hiyo ni kutokana na maandalizi katika mechi za makundi ya kufuzu fainali za michuano ya kombe la mataifa Africa (AFCON).
Pia timu hiyo itaondoka Tanzania kuelekea Misri mei 30 mwaka huu kuweka kambi ya siku saba kwa ajili ya mazoezi ambapo Juni 7 watarejea nchini.
Kocha Mayanga amewaita wafuatao kwenye timu hiyo.
Magolikipa: Aishi Manula (Azam FC), Beno Kakolanya (Yanga ) na Said Mohamed ‘Nduda’ (Mtibwa Sugar)
Mabeki: Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Hamisi ‘Kessy’ (Yanga), Mwinyi Haji, (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) Agrey Morris (Azam FC), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).
Viungo: Himid Mao (Azam FC), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Said Hamisi Ndemla (Simba), Mzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Farid Musa (Tenerife, Hispania), Shiza Kichuya (Simba), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden).
Washambuliaji: Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), Ibrahim Ajib (Simba) na Abdulrahman Musa (Ruvu Shooting).

Comments
Post a Comment