Mbao yasalimu amri kwa Azam.


Mei 7, 2017

Timu ya Mbao FC imekubali kipigo cha bao 3-1 kutoka kwa Azam FC katika uwanja wa Chamanzi Complex.

Ushindi huo umekamilisha kisasi dhidi ya Mbao ambayo iliichapa Azam bao 4 katika raundi ya kwanza ya ligi kuu katika uwanja CCM Kirumba Mwanza.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na John Bocco pamoja na Shaban Idd aliyerudi kambani mara mbili.

Azam inazidi kujihakikishia nafasi ya 3 kwenye ligi kuu baada ya kukusanya jumla ya pointi 49 ikiwa imebakiwa na michezo miwili pekee katika ligi ya Vodacom.

Comments