Nahodha wa Simba SC Jonas Mkude atajiunga na timu ya taifa baada ya kuruhusiwa na daktari katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mkude alipata ajali ya gari katika eneo la dumira mkoani Morogoro alipokuwa akirudi Dar es Salaam akitokea Dodoma katika fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Mbao FC na mtu mmoja alifariki kwenye ajali hiyo,
Hata hivyo alithibitisha kuwa Nahodha huyo wa Simba alipata mshtuko kidogo na kuchubuka katika baadhi ya maeneo ya mwili wake hasa eneo la shingo.
Baada ya kufanyiwa vipimo vyote nahodha huyo ameruhusiwa kuungana na wenzie katika kikosi cha timu ya Taifa cha mwalimu Salum Mayanga.

Comments
Post a Comment