Mei 7, 2017
Newcastle United chini ya Rafael Benitez imemaliza salama kwenye ligi ya Championship na kuongoza msimamo wa ligi hiyo.
Newcastle imeshinda bao 3-0 dhidi ya Burnsley na Mpinzani wake Brighton Hove and Albion wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Aston Villa.
Brighton ingeweza kuwa kinara wa ligi endapo ingeshinda mchezo wa Leo, na matokeo yanamfanya Newcastle kuongoza kuongoza kwa pointi moja mbele ya mpinzani wake.
Newcastle imemaliza ligi hiyo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 94 ikifuatiwa na Brighton yenye pointi 93 katika michezo 46 ya ligi hiyo.

Comments
Post a Comment