May 19, 2017
Chama cha soka nchini England maarufu kama FA wameaumua kuingia na mkakati kabambe wa kutoa adhabu kwa wachezaji wanaopenda kujiangusha kwa ajili ya kuzitafutia timu zao matokeo ya ushindi.
Kujiangusha kwa wachezaji kimekuwa kitendo kinachokera katika ligi mbali mbali duniani na kuumiza timu pamoja na mashabiki waliotendewa.
Kupunguza tatizo hilo chama cha soka England kimeamua kuja na mpango kabambe wa kutoa adhabu ya kukosa mechi mbili kwa mchezaji atayepatikana na hatia hiyo kuanzia msimu ujao wa ligi.
Matukio hayo yameonekana kuzigharimu timu nyingi kwenye ligi ikiwemo penati ya uongo ambayo ilitafutwa na mshambuliaji Marcus Rashford wakati Man utd ilipochuana na Swansea April mwaka huu.

Comments
Post a Comment