Mei 3, 2017
Klabu ya Simba kupitia Raisi wake Evans Aveva imesema kuwa itakwenda ngazi za juu kudai haki yao baada ya kupokwa pointi tatu ambazo zilirejeshwa katika timu ya Kagera.
Aveva alisema TFF ilikiri wazi kuwa Mohamed Fakhi alikuwa na kadi 3 za njano na hivyo hakukuwa na Sababu ya kunyimwa haki yao.
"Kanuni iko wazi nadhani lilikuwa ni suala la sisi kupokea pointi zetu kama kanuni inavyosema.
"TFF inadai rufaa haikuwasilishwa ndani ya saa 48, hatulipia ile rufaa na kuhusishwa kwa mjumbe asiyehusika kwenye kamati, pamoja na yote kanuni inabaki pale pale tulistahili kupata haki yetu." Alisema Aveva mbele ya waandishi wa habari.
Pia raisi huyo aliongeza kuwa Simba ipo tayari kwenda ngazi za juu ikiwemo FIFA na mahakani ya kimichezo.
Comments
Post a Comment