Ranieri atamani tena kufundisha soka England.


May 24, 2017

Aliyekuwa kocha wa Leicester City Claudio Ranieri anavutiwa na mpango wa kurudi England na kufundisha soka katika moja ya timu kwenye ligi hiyo.

Hadi sasa zipo timu mbili zenye mpango wa kusaka kocha mapya katika timu ya Watford na Crystal ambapo makocha wa timu hizo wamejiuzulu.

Walter Mazzari (Watfrod) na Sam Allardyce (Crystal Palace) wamejiuzulu kwenye nyazifa zao na timu zote mbili zimeingiza jina la Ranieri kwenye orodha ya makocha wanaohitajika.

Ranieri mwenye miaka 65 aliong'olewa katika timu ya Leicester mwezi wa pili mwaka huu kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Comments