May 27, 2017
Azam kupitia msemaji wake Jaffar Idd wamethibitisha kuwa aliyekuwa nahodha wa timu hiyo John Bocco si mali ya timu hiyo tena.
Hadi kufika leo taarifa mbali mbali zilikuwa zimeenea kwa John Bocco kuhusishwa na kujiunga na timu ya Simba.
Kupitia msemaji wa Azam imethibitika kuwa John Bocco amemaliza mkataba wake Azam na sasa ni mchezaji huru.
Idd alisema kuwa kuhusiana na taarifa za Bocco kujiunga na Simba wanatakiwa kumtafuta Bocco mwenyewe kwa kuwa hausiani na Azam kwa sasa.

Comments
Post a Comment