May 18, 2017
Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 "Serengeti Boys" leo imepata ushindi wa kwanza katika michuano ya kombe AFCON.
Serengeti boys imenasa pointi 3 baada ya kuichapa Angola bao 2-1 na kujihakikishia jumla ya pointi 4 katika michezo miwili ya makundi.
Serengeti boys ilitoka sare na Mali katika mchezo wa kwanza na itakuwa na kibarua cha mwisho dhidi ya Niger katika mchezo wa kuaga hatua za makundi.

Comments
Post a Comment