Serengeti Boys yamkaba koo bingwa mtetezi.


May 16, 2017

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti boys imetoa sare isiyokuwa na magoli dhidi ya Mali ambaye ndiye bingwa mtetezi wa michuano ya AFCON.

Serengeti ilionekana kujipanga vizuri katika safu ya ulinzi kwa vipindi vyote viwili vya mchezo huo na kuilazimisha Mali sare.

Kipindi cha pili Serengeti ilionekana kujipanga vizuri na kuongeza hali kujiamini uwanjani tofauti kidogo na kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Licha ya kukosa ushindi bado inabaki kuwa hatua nzuri kwa hao ambao bado wana kibarua kizito dhidi ya Niger.

Comments