Mei 4, 2017.
Klabu ya Simba kupitia rais wao Evans Aveva imesema kuwa hawana pingamizi juu ya uwanja uliotajwa na TFF kwa ajili ya mchezo wa fainali Dhidi ya Mbao.
TFF kupitia msemaji wake Alfred Lucas ilithibitisha kutumika kwa uwanja wa Jamuhuri uliopo mkoani Dodoma.
Pamoja na maamuzi hayo hata hivyo uongozi wa Simba ulisema kuwa bado TFF inatakiwa kufanya mambo yake kimataifa na kwa kufuta utaratibu maalum kama ilivyo katika ligi za nje.
"Hatuna pingamizi juu ya uwanja wa Jamuhuri isipokuwa TFF ifanye jitihada kuendesha mambo yake kama ligi zingine huko nje wanavyofanya.
"Kwenye ligi zingine maandalizi ya viwanja hufanywa kabla ya kuanza kwa ligi husika angalia ligi zote kubwa hufanya hivyo, mfano England kombe la FA, uwanja hufahamika kabla." Alisema Aveva ambaye ni rais wa Simba.
Mbali na suala uwanja pia Simba iligusia suala juu ya kupata haki yao kutokana na Fakhi kushiriki mechi yao akiwa na kadi 3 za njano.

Comments
Post a Comment