Ukata waimaliza Ndanda FC.


Wachezaji wa timu ya Ndanda FC ya Mtwara hawataingia uwanjani kutokana na kukosa malipo ya mishahara yao.

Wachezaji wa timu hiyo wanakabiliwa na hali mbaya kiuchumi hali inayopelekea kukosa pesa za kujikwimu katika maisha ya kawaida.

Hali ya kiuchumi katika timu hiyo haikuwa sawa tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom ambapo palikuwa na malalamiko mbali mbali ndani ya timu hiyo.

Wachezaji wa timu wametishia kugoma kuichezea timu hiyo iliyobakiza idadi ya mechi mbili kabla ya kumaliza kwa ligi ya Vodacom msimu huu.

Comments