West Ham yaiharibia Spurs mbio za Ubingwa.


Mei 6, 2017

Timu ya West Ham United imepunguza kasi ya Tottenham kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Olympic.

Bao pekee la West Ham United lilifungwa katika dakika ya 65 ya mchezo na kiungo machachali Manuel Lanzini.

Spurs itakuwa imetengeneza pengo la pointi 7 endapo Chelsea itashinda dhidi ya West Brom wikiendi hii na kuendelea ikiwa ni hatua nzuri katika mbio za ubingwa.

Comments