Xhaka, Welbeck waikalisha Man Utd.


Arsenal imepata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Emirates ukiwa ni mchezo wa marudiano kati ya timu hizo kwenye ligi ya EPL.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na kiungo wa timu hiyo Granit Xhaka katika dakika ya 53 na mshambuliaji wa zamani wa Man Utd Danny Welbeck aliyefunga dakika ya 57.

Wenger ameandika historia ya kumfunga Jose Mourinho kwa mara kwanza katika michuano ya ligi kuu England.

Comments