May 20, 2017
Licha ya kupoteza mchezo wa leo dhidi ya Mbao FC, Yanga wamefanikiwa kutetea na kulinda ubingwa wao kwa mara ya tatu.
Yanga inaweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara 3 mfulilulizo katika msimu wa 2014/15, 2015/16 na 2016/17 bila upinzani.
Pamoja na Simba kuanza vizuri msimu huu hata hivyo mabingwa hao waliweza kutumia vema udhaifu wa wapinzani wao Simba katika mechi ya mwisho.
Yanga na Simba zimefungana kwa pointi 68 hata hivyo idadi kubwa ya magoli inaifanya Yanga kuwa bingwa kwa mara ya tatu mbele ya mpinzani wake Simba.
Huu ni msimu wa 5 sasa wekundu hao wa msimbazi weshindwa kutwaa taji hilo licha ya kuonekana kuanza vizuri msimu huu.

Comments
Post a Comment