Yanga Yaingia mkataba na Sportpesa


May 17, 2017

Hatimaye mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC yaunga tela baada ya kusaini mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya bilioni 5 na kampuni ya ubashiri Sportpesa.

Mkataba huo umeisainiwa katika makao makuu ya timu hiyo mtaa wa jangwani wakishuhudiwa na waandishi wa habari waliohudhuria kwenye ofisi hizo.

Yanga itapokea kiasi cha shilingi milioni 950 kwa mwaka sawa na Simba ambayo imefanya marekebisho wa mkataba wao na kampuni hiyo.

Yanga inakuwa timu ya pili kusaini mkataba na kampuni hiyo baada Simba kufanya hivyo siku chache zilizopita.

Comments