Zaha awakata maini Arsenal, Spurs.


Winga wa Crystal Palace amevunja matumaini ya kusajiliwa na majirani zake wa London baada ya kusaini dili jipya la miaka 5 ndani ya timu hiyo.

Zaha mwenye miaka 24, alikuwa akihusishwa kusajiliwa na baadhi ya timu ambazo zilikuwa zikimtolea macho ikiwemo Arsenal, Tottenham.

Raia huyo wa Ivory Coast amekuwa na msimu mzuri na Crystal Palace ambayo ameifungia jumla ya magoli 37 hadi sasa.

Zaha aliongeza kuwa ana furaha kubwa 
kuitumikia timu yake hiyo ambayo ilimkuza tangu alipokuwa mchanga katika soka.

"Nina furaha kuwa hapa, na moyo wangu upo Palace" Alisema zaha baada ya kukanusha madai ya kujiunga na Tottenham.

Comments