Aguero hana mpango wa kuondoka City.


Mshambuliaji wa Manchester city Sergio Aguero amesema kuwa hana mpango wa kuondoka kwenye timu hiyo kwa sasa.

Fowadi huyo ameifungia Manchester city mabao 33 katika mechi 45 ambazo Aguero ameichezea city kwenye  mashindano yote msimu uliomalizika.

"Bado nina miaka miwili ndani ya mkataba wangu, nataka kubaki city, nina furaha kuwa hapa." Alisema Aguero

"Nafikiri nilikuwa na msimu mzuri, na hata kiwango changu kilikuwa bora, ni ukweli usiofichika nilikosa mechi nyingi na hii imenifanya kupoteza magoli mengi sana." Aliongeza fowadi huyo.

Comments