Ake wa Chelsea avunja rekodi ya usajili Bournemouth.


Aliyekuwa beki wa Chelsea Nathan Ake ametua AFC Bournemouth kwa dauni la pauni 20 milioni.

Mholanzi huyo mwenye miaka 22 amevunja rekodi ya usajili ya mchezaji Jordon Ibe ambaye alitua kwenye timu hiyo kwa ada ya uhamisho wa pauni 15 milioni.

Ake alitumia nusu msimu ulioisha akiwa mchezaji wa mkopo katika timu hiyo baada ya kutokea Watford alipokuwa kwa mkopo pia na kurejeshwa Chelsea kipindi cha January.

Comments