Ally Mayai azama kuwania Urais TFF.


Mchezaji wa Zamani wa Yanga SC na timu ya Taifa ya Tanzania Ally Mayai amechukua ya kugombea nafasi ya Urais TFF.

Ally ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya soka katika kituo cha Azam Tv alifika katika ofisi hizo akiongozana na mchezaji wa zamani Ramadhani Katemi ambaye alichukua fomu katika nafasi ya makamu wa rais.

Kwa pamoja Ally na Katemi walisindikizwa na wadau mbali mbali wa soka akiwemo Kicha Jamuhuri Kihwelo 'Julio' na Bakari Malima 'Jembe Ulaya'.

Comments