Mchezaji wa Zamani wa Real Madrid Alvaro Arberoa ametangaza kustaafu soka baada ya kuachwa na West Ham ya England.
Arberoa mwenye miaka 34 alicheza mechi tatu pekee tangu alipojiunga na West Ham akitokea Real Madrid hapo mwaka jana.
Raia huyo wa Hispania alisema kuwa bado mwili wake unadi lakini ameamua kuangalia mambo mengine kwenye maisha.
"Sijachoka mwili, bado nipo vizuri, nimeamua kustaafu soka ili kupisha mambo mengine kwenye maisha." Alisema Arbeloa.
Beki huyo amewahi kuichezea Liverpool kwa miaka 3 na mwaka 2009 alijunga na Real Madrid na kufanikiwa kubeba taji la ligi kuu Hispania mara moja na taji la ligi ya mabingwa mara 2.
Pia mkongwe huyo amewahi kunyanyua ubingwa wa kombe la dunia akiwa mmoja wa wachezaji waliounda kikosi cha timu ya taifa ya Hispania mwaka 2010.


Comments
Post a Comment