Timu ya Arsenal, imeanza mazungumzo na timu ya Olympic Lyon kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji Alexandre Lacazette.
Timu ya Olympic Lyon ilikataa ofa £29 milioni ikiyotolewa na Arsenal hapo awali kama ada ya uhamisho wa mchezaji ambapo ilithibitisha kuwa thamani ya Lacazette ni £44 milioni.
Hapo awali mchezaji huyo aliweka makubaliano ya kutua Atletico Madrid lakini imeshindikana baada ya klabu hiyo kukumbana na adhabu inayowazuia kusajili.
Lacazette amefunga jumla ya mabao 37 katika mechi 45 alizoichezea Lyon msimu uliopita na pia mchezaji huyo amefunga magoli 119 kati ya mechi zaidi ya 200 ambazo ameichezea Lyon.

Comments
Post a Comment