Aubameyang abadili upepo Old Trafford.


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amepiga chini mpango wa kumsajili Antoinne Griezman na kuhamishia makali kwa Pierre-Emerick Aubameyang.

Aubameyang mwenye miaka 28 ndiye aliyeibuka kinara wa mabao katika ligi ya Bundesliga baada ya kumpiga chini mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski.

Griezman hajapokea kwa bashasha taarifa za kufukuziwa na mashetani hao wekundu na sasa Mourinho amehamishia jeshi la lake la Usajili kwa raia huyo wa Gabon.

Hadi sasa hakuna uhakika ya huduma ya Zlatan Ibrahimovic pamoja na Wayne Rooney hali inayopelekea Mourinho kumfukuzia nyota huyo.

Comments