Azam FC imefanya usajili wa kwanza.


Klabu ya Azam FC imeanza mipango ya usajili kuimarisha kikosi chake tayari imenasa saini ya mshambuliaji wa Toto African Wazir Junior ambaye amesaini miaka 2.

Mshambuliaji huyo mwenye mabao 6 ni pendekezo la kocha wa sasa wa timu hiyo Aristica Cioaba ambaye alivutiwa na kiwango chake kwa muda mrefu.

Waziri Junior alisaini mkataba huo jana katika ofisi za timu hiyo chini ya Meneja mkuu wa timu hiyo Abdul Mohammed, na viongozi wengine wa timu akiwemo Jaffar Idd ambaye ni msemaji wa Azam pamoja na baadhi ya waandishi wa habari.

Comments