Azam FC imesajili wengine wawili.


Timu ya Azam FC imeendelea kufanya makubwa katika dirisha la usajili baada ya kunasa saini za wachezaji wengine wawili.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Kagera Sugar 
Mbaraka Yusuph na Kiungo wa Mbao FC ambaye alikuwa muhimili kwa wababe hao wa Mwanza Stamili Hoza wote kwa pamoja wamesaini miaka miwili.

Mbaraka na Stamili wanakamilisha idadi ya wachezaji watatu ambao wamesajiliwa na Azam mpaka sasa baada ya kufanya kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Toto Africa Waziri Junior.

Comments