Bakayoko, Sandro usajili wa kwanza Chelsea.


Chelsea imeanza mazungumzo na kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko pamoja na Beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro.

Bakayoko alisajiliwa na Monaco miaka miwili iliyopita kwa dau la £7 milioni na sasa wanampiga bei kwa dau la £35 milioni.

Hadi sasa kiungo huyo mwenye miaka 22 ameichezea AS Monaco mechi 51 tangu alipotua kwenye timu hiyo mwaka 2015.

Mbali na Bakoyoko pia Chelsea imejipanga kumnasa Alex Sandro ambaye alisajiliwa na Juventus miaka miwili iliyopita akitokea FC Porto ya Ureno kwa dau la £23 milioni.

Beki huyo ambaye ni raia wa Brazil thamani yake £51 milioni ambayo Chelsea inapaswa kulipa kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo.

Comments