Bayern kumfanya Sanchez anayelipwa zaidi Bundesliga.


Timu ya Bayern Munich ya Ujermani inajiandaa kuweka ofa nono ya mshahara ili kuinasa saini ya Alexis Sanchez kutoka Arsenal.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily mirror Sanchez ndiye atakayelipwa zaidi kwenye ligi baada ya kuhaidiwa mshahara mnono wa paundi 350000 kwa wiki.

Mbali na Bayern, Man city na Chelsea zipo kwenye ushindani wa kuwania saini ya mchezaji huyo ambaye anapokea kiasi cha dola milioni 11.5 kwa mwaka katika timu ya Arsenal.

Comments