Mwenyekiti wa timu ya Tottenham Daniel Levy amesema kuwa hatapokea simu zinazohusiana na mpango wa kumpiga bei strika wa timu hiyo Harry Kane.
Kauli ya mwenyekiti huyo imeonesha wazi kuwa Spurs haina mpango wa kuachana na nyota huyo wa England ambaye amekuwa tishio kwenye ligi ya EPL.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anavutiwa na mpango wa kumsajili Harry Kane aliyebeba kiatu cha dhahabu kwa misimu miwili mfululizo katika ligi ya England.
Harry Kane aliweza kuifungia timu yake mabao 29 katika ligi ya EPL pekee licha ya kupatwa na majeraha yaliyomuweka nje mara kadhaa.

Comments
Post a Comment