Cheick Tiote afariki Dunia akiwa mazoezini.


Aliyekuwa kiungo wa zamani wa Newcastle United Cheick Tiote amefariki dunia akiwa mazoezini nchini China.

Kiungo huyo alianguka ghafla akiwa na kikosi cha Beijing Enterprises ambayo ilimsajili kiungo huyo February mwaka huu.

Tiote amefariki akiwa na umri wa miaka 30 na tayari ameichezea timu yake ya taifa idadi ya mechi 156 hadi umauti ulipomkuta.

Raia huyo wa Ivory Coast alisajiliwa Newcastle mwaka 2010 akitokea FC Twente ya Uholanzi kwa dau la £3.5 milioni kama ada ya uhamisho.

Comments