Manchester United imekamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa Benifica Victor Lindelof ambaye amesaini miaka 4 kwa dau la £30 milioni.
Liverpool imeambiwa inatakiwa kuongeza dau la £10 milioni katika ile ofa ya £26 waliyotoa kwa usajili ya kufanikisha usajili wa Mohamed Salah kutoka AS Roma.
Barcelona bado ina matumaini ya kumnasa kiungo wa PSG Marco Verratti ambaye bado anahitajika na timu yake.
Dogrus Costa ameitaka Juventus kupeleka ofa kwa Bayern Munich ili kukamilisha usajili wake kutua Turin.
Swansea inavutiwa na mpango wa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Emanuel Adebayor.
Mshambuliaji wa Monaco Kylan Mbappe amesema kuwa anahitaji muda ili kuamua hatma yake, kubaki Monaco au kutimka.

Comments
Post a Comment