AMEREJEA: Hanspoppe amalizana na Okwi.


Mwenyekiti kamati ya usajili Simba Zakaria Hanspoppe ni kama amekamilisha dili la usajili wa Emanuel Okwi baada ya kusafiri Kampala nchini Uganda.



Hanspoppe alionekana jijini Kampala na nyota huyo ambaye amewahi kufanya vizuri kwa kipindi chote alichowahi kuwa ndani ya klabu ya Simba.

Simba imempoteza Ibrahim Ajib ambaye ametua Yanga na Okwi anatua Msimbazi kwa mara nyingine.

Comments