Himid ndiye kipenzi cha mashabiki Azam.


Kiungo mkabajiwa wa Azam FC Himid Mao Mkami ndiye mchezaji anayependa zaidi baada ya kuzoa kura nyingi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.

Himid alizoa kura 151 ikiwa ni nusu nzima kati ya kura zote 293 ambazo zilipigwa na mashabiki hao kupitia kurasa za Facebook na Instagram zinazomilikiwa na Azam FC.

Beki wa Azam Jakub Mohamed ndiye aliyemfuata Himid baada ya kupata kura 72 na mshambuliaji Shaaban Idd ambaye alifunga tamati ya zoezi hilo baada ya kujizolea kura 70.

Comments