Hivi ndivyo washambuliaji wa Ufaransa wanavyotikisa kwenye usajili.


Ufaransa ni kama imeshushiwa neema kwa sasa kutokana na washambuliaji wake kutikisa soko la usajili kwa sasa.

Kylan Lotten Mbappe, Antonio Griezmann na Alexander Lacazzete ndiyo wanaotikisa sokoni kwa sasa na kuzitoa macho klabu kubwa barani ulaya.

Kylan Mbappe.

Kijana huyu mwenye miaka 19 anatikisa sasa kwenye soko la usajili baada ya kufanya vizuri katika kikosi cha Monaco. Mbappe ameingoza Monaco kutwaa taji la ubingwa wa ligi kuu na kuingia kwenye nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Thamani yake inakadiliwa kufikia £100 milioni katika soko la usajili, Real Madrid, Liverpool na Arsenal zimeonesha nia ya kumsajili.

Antonio Griezmann.

Hakuna ubishi juu ya ubora wa Griezmann (26) ambaye amekuwa muhimili mkubwa katika timu ya Atletico Madrid. Thamani ya Griezmann inakadiliwa kufika £150 milioni. Hadi sasa Man Utd inaongoza katika mbio za kumwania nyota huyu.

Alexander Lacazette.

Ni mshambuliaji bora kwa sasa katika timu Olympic Lyon, Lacazette (26) ana uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu na kujitengeneza thamani katika soko la usajili. Mchezaji huyo anafikia thamani £75 milioni.

Manchester United, Chelsea na Arsenal huenda zikawa vitani kumwania mchezaji huyo.

Comments