Kiungo wa Yanga Thabani kamusomoko amewataka mashabiki wa timu hiyo kuondoa hofu juu yake kwani ataendelea kuichezea timu hiyo.
Raia huyo wa Zimbabwe amesema kuwa mashabiki wa Yanga waondoe hofu kwani yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.
"Ingawa nimepokea ofa nyingi nyumbani Zimbabwe, Tanzania na baadhi ya nchi nyingine lakini hamu yangu ni kuendelea kuichezea Yanga.
"Bado kuna mambo sijatimiza ndani ya klabu hii, tuna kibarau cha kusaka ubingwa wa klabu bingwa Afrika hivyo nina deni ndani ya Yanga." Alisema Kamusoko
Pia kiungo huyo aliongeza kuwa ana imani na wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo na hivyo ana imani wataendelea kufanya vyema.
Source; Goal.com
Source; Goal.com

Comments
Post a Comment