Uongozi wa Ruvu Shooting umejiridhisha kufanya mazungumzo Shaban Kisiga kwa ajili ya kumpatia mkataba mpya kiungo huyo.
Kisiga amemaliza mkataba wake na maafande hao na tayari uongozi wa timu umeridhika na kiwango chake.
Msemaji wa Timu hiyo Masau Bwire amesema kuwa mazungumzo kati ya Uongozi na mchezaji huyo yanaendelea vizuri.
"Kisiga ni mchezaji mzuri na ameonesha mapenzi ya kuendelea na timu yetu.
"Mazungumzo kati yetu yanaendelea vizuri, na muda na muda wowote Kisiga atasaini mkataba mpya." Alisema Masau Bwire.
Comments
Post a Comment