Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa kati wa Toto Africans Yusuph Mpili ambaye amesaini miaka 3 kwenye timu hiyo.
Simba imekosa mtu sahihi wa kuimairisha na kuongoza beki yao tangu alipoumia kitasa wa timu hiyo Method Mwanjali ambaye ni raia wa Zimbabwe.
Zoezi hilo lilifanyika jana katika ofisi za Simba ambapo beki huyo alisaini mkataba mbele ya makamu wa raisi wa Simba Geoffrey Kaburu.

Comments
Post a Comment