Kiungo hatari wa Ajax atua Everton.


Timu ya Everton imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Ajax Davy Klaassen ambaye amesaini miaka 5 kwa dau la paundi 23.6 milioni.

Mholanzi huyo mwenye miaka 24 ameifungia Ajax mabao 49 katika mechi 163 alizoichezea timu tangu alipojiunga na timu mwaka 2011 na kunyanyua mataji matatu ya ligi kuu.



Ronald Koeman ambaye ni kocha wa Everton amefanya usajili huo baada ya Ross Barkley kukataa kumwaga wino kwenye mkataba mpya.

Klaassen anakuwa mchezaji wa pili kutua Everton zikiwa zimepita siku mbili tangu kukamilika kwa usajili wa golikipa Jordan Pickford kutoka Sunderland.

Comments