Kiungo wa zamani aliyeweka heshima kubwa Chelsea Frank Lampard amesema kuwa timu hiyo itakuwa imefanya jambo jema endapo itamsajili Romelu Lukaku.
Lampard ana imani kuwa Chelsea inahitaji kupata mtu sahihi endapo imeamua kwa dhati kuachana na Diego Costa.
Kwa upande wa Lampard anamtazama Lukaku kama mshambuliaji aliyekomaa na ameunga mkono chaguo la Antonio Conte.
Pia kiungo huyo amewahasa Chelsea kuwa makini sokoni ili kujihakikishia nafasi sahihi ya kumnasa Lukaku mwenye miaka 24.

Comments
Post a Comment