Lindelof akaribia kutua Man United.


Manchester United imefikia makubaliano na Benifica kuhusiana na ada ya uhamisho wa beki Victor Lindelof.

Benifica imekubali kumuachia Lindelof baada ya kufika makubaliano ya dau la £30.7 milioni kama ada ya uhamisho wa beki huyo wa kati.

Lindelof ambaye ni raia wa Sweden atatua Man Utd muda wowote kuanzia sasa baada ya kumalizana na Man utd kuhusiana na maslahi binafsi.

Comments