Mancini arejea kibaruani.


Aliyewahi kuwa kocha wa Manchester city Roberto Mancini amesaini miaka mitatu kukinoa kikosi cha wababe wa Urusi Zenit St Petersburg.

Mancini ambaye raia ni wa Italy aliondelewa kwenye kikosi cha Intermilan mwaka jana kutokana na maelewano mabovu na tajiri wa timu hiyo.

Baada ya kuadimika kwa kipindi cha mwaka mmoja hatimaye kocha huyo amerejea kazini rasmi.

Mbali na Mancity, Mancini amewahi kuzinoa timu kadhaa ikiwemo Intermilan ya Italy na Galatasaray ya Uturuki.

Comments