Matola apata shavu la kuinoa Lipuli FC.


Aliyewahi kuwa mchezaji na kocha wa vijana katika klabu ya Simba Suleiman Matola ametangazwa kuwa kocha mpya wa Lipuli ya Iringa kwa mkataba wa mwaka mmoja.


Awali kocha huyo aliondoka Simba baada ya  kupata kibarua katika timu ya Geita Gold Mining ambayo ilikumbwa na kashfa ya kupanga matokeo.

Lipuli FC imeungana na Njombe Mji pamoja na timu ya Singida United ambazo kwa pamoja zitashiriki ligi kuu baada ya kupanda daraja.

Kwa upande wa Matola amesema kuwa mipango yake kwa sasa ni kusajili wachezaji vijana ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Comments