Baba wa Jose Mourinho afariki dunia.


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amefiwa na baba yake mzazi Mzee Felix Mourinho aliyekuwa na umri wa miaka 79.

Mzee Felix Mourinho alifariki siku ya jumamosi lakini hata hivyo chanzo cha kifo cha kifo chake hakijawekwa wazi kwenye vyombo vya habari.

Felix Mourinho aliwahi kuwa golikipa wa zamani wa timu ya Vitoria Sebutal ambayo ilitinga fainali ya kombe la Ureno dhidi ya Benifica 1965.

Comments