Winga wa Azam Ramadhani Singano 'Messi' huenda akaachana na Azam FC baada ya kushindwa kufikia makubalino ya mkataba mpya.
Azam ambayo kwa sasa imeingia kwenye mfumo wa kubana matumizi imegoma kutoa kutoa kiasi cha shilingi milioni 40 ambacho anakihitaji mchezaji huyo.
Singano amekataa kiasi cha shilingi milioni 10 na punguzo la mshahara wa awali kiasi cha milioni 2,000,000 hadi shilingi 1,500,000.
Endapo Singano ataondoka Azam atakuwa ameungana na baadhi ya nyota ambao pia wameondoka Azam akiwemo John Bocco, Shomari Kapombe na Aishi Manula ambao wamejiunga na Simba.

Comments
Post a Comment