Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Craig Bellamy ameipa tano timu hiyo baada ya kufanikisha usajili wa Mohamed Salah.
Bellamy alisema kuwa Salah ni mchezaji bora ambaye ataendana na mtindo wa kocha wa sasa wa Liverpool, Jurgen Klopp.
"Ni usajili mzuri, Liverpool imepatia kumsajili, alinivutia tangu alipokuwa FC Basel.
"Alistahili kutua Chelsea wakati ule, ingawa mambo hayakuwa mazuri sana lakini bado alipata nafasi ya kuonesha ubora wake alipojiunga na AS Roma." Alisema Bellamy.

Comments
Post a Comment