Nyoso arejea uwanjani, amfata Mexime Kagera.


Aliyewahi kuwa beki wa Simba Juma Nyoso amerejea uwanjani baada ya miaka miwili ya adhabu na kujiunga na timu ya Kagera Sugar.

Nyoso alifungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na kitendo cha utovu wa nidhamu alichokifanya kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC John Bocco.

Mbali na Juma Nyoso wengine walijiunga na Kagera Sugar ni pamoja na Peter Mwalyanzi na Venance Ludovic ambao wote kwa pamoja wametokea African Lyon.

Comments