Nyota watano wenye soko Series A.


Kama ilivyo kawaida wakati dirisha kubwa la usajili likiendelea kupamba moto Eskaone blog imekuwekea machoni nyota watano wanaocheza kwenye ya Serie A (Italy) ambao wanaongoza kuwindwa sokoni.

Mohamed Salah 

Raia huyu wa Misri ameifungia AS Roma mabao 19 katika msimu uliomalizika na kuiwezesha
Roma kufuzu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Awali Liverpool ilipeleka dau la paundi 26 milioni ili kuinasa saini ya mchezaji huyo. Hata hivyo Roma imewaambia Liverpool iongeze dau la mchezaji hadi kufikia paundi milioni 35.

Carlos Bacca 

Bacca ameifungia Milan mabao 13 katika msimu uliomalizika na bado anaonesha yupo kwenye kiwango cha hali ya juu. klabu ya Everton kutoka Uingereza ndiyo inayoongiza kumwania nyota huyo ambaye ni raia wa Colombia.

Ivan Perisic

Winga huyu mwenye miaka 28 anafukuziwa kwa udi na uvumba na klabu ya Manchester United, amekuwa mchezaji mzuri na kuing'arisha Intermilan katika msimu uliomalizika. dau lake linakadiriwa kufikia paundi 40 milioni. Manchester United inakibarua kizito cha kushindana na Paris Saint Germain (PSG) ambayo nayo inamtolea macho nyota huyo wa Croatia.

Andrea Belloti 

Hakuna shaka juu ya ubora wa Belloti mwenye miaka 23 ambaye alifunga mabao 26, akiachwa mabao matatu na aliyekuwa kinara wa mabao katika ligi hiyo na  Edin Dzeko ambaye alifunga mabao 29. Belotti anatolewa macho na klabu kadhaa ikiwemo AC Milan, Chelsea na Manchester United.

Leonardo Bonucci 

Ubora wake unawafanya wengi wamtani na kuiwania saini yake. Amekuwa muhimili mkubwa katika ukuta wa timu Juventus na mshirika wake Giorgio Chiellin. Antonio Conte wa Chelsea anamsaka kwa udi na uvumba mchezaji huyo ambaye aliwahi kumnoa alipokuwa kocha wa Juventus.



Comments