Okwi amwaga wino Simba SC.


Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emanuel Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba SC.

Okwi alitua jana na tayari amekamilisha mpango wa kuingia rasmi kwenye kikosi cha Simba baada ya kukamilisha zoezi hilo ambalo lilisimamiwa na makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange.

Mshambuliaji anarejea Simba kwa mara ya tatu baada ya kuitumikia timu hiyo katika vipindi tofauti hapo nyuma.

Comments