Okwi anahesabu siku 2 kutua Simba.


Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Uganda Emanuel Anold Okwi atakuja nchini baada ya siku mbili kumalizana na klabu ya Simba SC.

Okwi alionekana na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspoppe wiki iliyopita katika jiji la Kampala nchini Uganda.

Simba inaonekana kupania kufanya vizuri katika ligi kuu na michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambapo mpaka sasa Okwi anatarajiwa kuwa mchezaji wa 9 kati ya nane waliosajiliwa.

Mbali na Okwi, zipo tetesi kuwa aliyekuwa kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima pamoja na Mshambuliaji Donald ngoma huenda wakatua Msimbazi.

Comments